Mfanyabiashara na Mdhamini wa Yanga SC Ghalib Said Mohammed (GSM) ameonesha nia ya kuona Rais wa TFF Wallace Karia na Haji Manara wanaelewana baada ya Julai 2 2022 kutofautiana katika mchezo wa fainali ya Kombe la ASFC lililozikutanisha timu za Yanga na Coastal Union katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.
Tukio hilo lilipelekea Haji Manara tarehe 21 Julai 2022 afungiwe na Kamati ya Maadili ya TFF miaka miwili kujihusisha na soka na faini ya Tsh milioni 20 kwa kukutwa na hatia ya kosa la kumkosea heshima Rais wa TFF na kumtolea maneno yasiofaa.
Hata hivyo 21 Julai 2024 Haji Manara atakuwa anatimiza miaka miwili toka afungiwe kujihusisha na soka na atakuwa ana maliza adhabu, ambapo baadhi ya viongozi wa soka nchini wanadai kuwa hakuitumikia adhabu hiyo.