Kampuni ya GSM Spareparts ambayo ni moja kati ya makampuni ya GSM GROUP imezindua rasmi bidhaa mpya ya kilainishi cha pikipiki na bajaji iitwayo GSM SPEEDY 4T. Uzinduzi huo umefanyika rasmi jijini Dar es Salaam katika moja ya maduka ya GSM Spareparts lililopo mtaa wa Lumumba Kariakoo.
“GSM spareparts inaendelea kutimiza ahadi ambayo iliwekwa tangu kuanzishwa kwake zaidi ya miaka mitano nyuma katika kuhakikisha inaleta bidhaa ambazo zina ubora na tija kwa waTanzania” alisema hayo meneja masoko Bi. Rukia Yazid. Aliendelea na kusema “kwetu sisi hii ni hatua kubwa sana kama sehemu ya makampuni ya GSM GROUP ambayo kila leo tunaangalia fursa za biashara mbali mbali ili kukuza kampuni yetu, kuwa sehemu ya ukuaji wa kiuchumi na kuchangia kipato kwa serikali yetu.”
GSM Spareparts inaendelea kushirikiana na wataalamu wa uzalishaji wa vilainishi na vipuri vya magari katika kuleta bidhaa bora hapa nchini. “Ukiacha kazi kuu ya GSM SPEEDY 4T ambayo ni kulainisha engine, bidhaa yetu ina sifa ya kuboresha ufanisi wa engine pamoja na kuilinda iweze kudumu kwa muda mrefu, haya yote yanaifanya safari ya chombo chako isiwe na misuko suko.” Alisema haya meneja mauzo Yohana Bute. ALiongezea kwa kusema “Tunaelewa kuwa watumiaji wa vyombo kama piki piki na bajaji ni watu ambao wanajali sana muda wao kutokana na kuwa wengi wao wanatumia vyombo hivi katika kufanya biashara, hivyo basi napenda kuwahikikishia kuwa kilainishi cha GSM SPEEDY 4T ni rahisi kwa mtumiaji”
GSM SPEEDY 4T inapatikana nchi nzima katika maduka ya GSM Spareparts yakiyopo mtaa wa Lumumba, Kariakoo, Maduka mawili chang’ombe Pamoja na Tunduma. Vile vile bidhaa hii inapatikana kwa wasambazaji wa vipuri na vilainishi vya vyombo vya moto.
GSM spare parts imekuwa wasambazaji wa vipuri na bidhaa zingine za malori ya kichina, betri za magari, vilainishi na leo hii GSM Spare parts imetanua wigo wa biashara zake kujikita rasmi kwenye bidhaa za vilainishi za vyombo vya moto vya pikipiki na bajaji. GSM spareparts imewaomba wadau wake kuendelea kushirikiana nao katika biashara ili kuweze kufikisha malengo yake ya kibiashara.