Club ya Man City Jumapili ya August 19 2018 ilicheza game yake ya Ligi Kuu England msimu wa 2018/2019 dhidi ya Huddersfield katika uwanja wao wa Etihad, Man City ambao ndio Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo jana walifanikiwa kupata ushindi wa magoli 6-1.
Baada ya game hiyo mshambuliaji wa Man City Riyad Mahrez ambaye alicheza pia game hiyo akitokea benchi dakika ya 64, baadae alirudi Lowry Hotel amapo anaishi kwa sasa akiwa na kundi la marafiki zake wakisherehekea ushindi huo.
Mahrez akiwa na rafiki zake walishuka katika gari aina ya Bentley yenye thamani ya pound 160000, wakati Riyad Mahrez akirudi hotel akiwa na furaha kutokana na ushindi huo, Man United wao walikuwa wametoka kupoteza kwa magoli 3-2 dhidi ya Brighton.
Kuingia hotelini kwa shangwe kwa Mahrez kumechukua headlines kwani wanaishi hotel moja na kocha wa Man United Jose Mourinho katika jiji la Man City ambapo Mourinho yeye ana majonzi kutokana na timu yake kupokea kipigo kwa timu inayodhaniwa kuwa kibonde.
Manji aibuka Yanga leo, asema ‘hakuna zawadi kubwa kama……….?’ (+video)