Kampuni ya Azam Marine na Kilimanjaro Fast Ferries inayojihusisha na usafirishaji wa vyombo vya baharini leo Jumanne ya October 23 2018 imetangaza rasmi kusitisha safari zake za boti kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar na kutoka Zanzibar kwenda Dar es Salaam.
Azam Marine wamefikia maamuzi ya kusitisha huduma hiyo kwa sababu Mamlaka ya usafiri wa Baharini (ZMA) inawatangazia abiria wote kusitishwa kwa safari zake kati ya Dar es Salaam na Zanzibar kwa kutumia vyombo vya Kilimanjaro kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya baharini.
Kutokana na taarifa kutoka mamlaka ya hali ya hewa ya Zanzibar uamuzi huo unaanzia leo October 23 na huduma itarudi kama kawaida endapo hali ya hewa itakaa sawa na kuthibitishwa na mamlaka ya hali ya hewa kuwa bahari sasa ipo shwari.
CHANZO: Azam TV
MAGAZETI: Mpya yaibuka sakata la MO, Waziri Makamba, Lema wahojiwa