SportPesa imeendelea kukabidhi Bajaji kwa washindi ambao wametupia ubashiri na kuingia kwenye Droo ya Shinda Zaidi na SportPesa na wakati huu timu hii ya ushindi iliweka kambi Mwera wilaya ya Pangani mkoa wa Tanga .
Hapa ilikuwa ni zamu ya mshindi wa Droo ya Kwanza kabisa Bwana Ntale Rajabu ambaye tayari amekabidhiwa bajaji yake zoezi ambalo lilisimamiwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani, Zainab Abdallah
Akizungumza wakati wa kumkabidhi bajaji hiyo kutoka SportPesa mkuu wa wilaya `pangani na kuwataka wananchi wa Pangani kucheza zaidi ili kupata washindi wengine zaidi.
“Leo tunashuhudia kwa Macho Baada ya Ntale kuwa mshindi kutoka hapa pangani naomba Hii iwe hamasa kwa wengine zaidi kucheza kwa sababu unaposhinda bajaj hii kutoka SportPesa ndio Mwanzo wa kubadili maisha tunawashukuru sana SportPesa kufanya mambo haya kwa vitendo na kwa uwazi mkubwa ” >>> DC Zainab
Kwa upande mwingine mshindi wa bajaji hiyo ya Droo ya Kwanza ya Shinda Zaidi na SportPesa, Ntale alishukuru sana kampuni hiyo ya michezo ya kubashiri hapa nchini kwa kueleza kuwa mwanzo hakuamini hadi alipoona timu ya SportPesa imefika mpaka nyumbani kwao ikiongozwa na mkuu wa wilaya.
SportPesa sio wa mchezomchezo, Bajaji 100 kwa siku 100