Pamoja na kuwa Bank ya CRDB imezidi kuboresha huduma zake na kurudisha fadhila kwa wateja wake, kupitia promotion yao ya Sim Account leo imeendeleza utaratibu wa kugawa zawadi ya pesa kwa wateja wanaotumia huduma ya Sim Account.
CRDB kwa sasa inaendesha promotion ya Sim Account na kwa kujisali tu kwa kubonyeza *150*62# na kufuata maelezo, basi namba yako moja kwa moja inaingia katika shindano la kushinda pesa kuanzia laki moja, milioni moja na milioni mbili kila wiki lakini Alhamisi ya mwisho wa mwezi wanatoa mshindi wa Tsh Milioni 10.
Taarifa ikufikie kuwa leo ndio Alhamisi ya mwisho wa mwezi kama ilivyokaida CRDB imechezesha droo ya kupata washindi wa zawadi ya Tsh Milioni 10 na Milioni tano, wiki ijayo wataendelea tena na shindano hili kwa kutoa zawadi ya Tsh Milioni mbili, milioni moja na laki moja pia.
“Tumeshinda ili kuweka tabasamu usoni kwa MO Dewji”-Kocha Simba SC