Moja kati ya habari kubwa katika mitandao ya kijamii ni kutoka nchini Ukraine kuhusiana na ushindi wa nafasi ya urais kwa mchekeshaji maarufu wa taifa hilo Volodymyr Zelensky kushinda nafasi ya ya Urais wa taifa hilo na kumshinda aliyekuwepo madarakani.
Ushindi wa Volodymyr Zelensky kuwa Rais mpya wa Ukraine Petro Poroshenko aliyekuwepo madarakani toka 2014, kumewashangaza wengi ukizingatia mchekeshaji huyo hana uzoefu wowote wa siasa na ameshinda kwa kishindo, Rais wa zamani wa Ukraine Petro Poroshenko amekubali kushindwa na ameahidi kumuunga mkono Zelensky.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari vya kuaminika barani Ulaya vinaelezwa kuwa Volodymyr Zelensky mwenye umri wa miaka 41 ameshinda nafasi hiyo ya Urais kwa asilimia 73, Zelensky alijizolea umaarufu kwa movie zake za vichekesho mbalimbali ikiwemo Servant of the People.
RPC Kilimanjaro athibitisha kukamatwa kwa askari anayetuhumiwa kwa mauaji