Katika ulimwengu wa soka kuna mechi chache sana zinazoweza kuamsha hisia kama derby ya Der Klassiker ambayo itapigwa Jumamosi hii katika dimba la Allianz Arena, ngome ya Bayern Munich, game hiyo ni zaidi ya derby ya kawaida kwa sababu timu zote mbili zinawania Ubingwa wa Bundesliga.
Borussia Dortmund walirejea kileleni mwa Ligi baada ya ushindi wa dakika za lala salama kwa mabao 2-0 dhidi ya Wolfsburg, huku Bayern wakidondosha alama mbili baada ya kutoka sare ya bao 1-1 ugenini kwa Freiburg, game hiyo itaifanya Bayern kupanda kileleni kwenye msimamo wa ligi endapo watashinda. Borussia Dortmund wao wanatakiwa kuepuka kufungwa ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa wa Bundesliga.
Dortmund watataka kujifunza kutoka kwa Liverpool wanaofundishwa na kocha wao wa zamani Jurgen Klopp ambaye aliwafunga Bayern wiki tatu zilizopita katika uwanja wao wa nyumbani Allianz Arena na kuwatoa katika hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League
Kocha wa Bayern anafahamu vizuri kuwa anahitaji ushindi dhidi ya Dortmund kwa gharama yoyote. Akiongea baada ya sare ya Freiburg alisem “Nadhani wachezaji wanajua nini tunatakiwa kufanya tunatakiwa kuwaonyesha Dortmund kwamba tunataka kuwa mabingwa naninatagemea tutacheza mchezo mzuri dhidi yao”
Bayern wametangaza usajili wa wachezaji wapya kwa msimu ujao kama vile Kai Havertz wa Bayer Leverkusen. Usajili wa aina hii unaweza kusaidia kuongeza au kupunguza morali kwa baadhi ya wachezaji kama Jerome Boateng ambaye anaweza kuhisi hahitajiki tena kikosini hapo hivyo kuathiri kiwango chake uwanjani, game hiyo itachezwa saa 19:30 kwa saa za Afrika Mashariki.
Wachezaji wa Dortmund wanaenda Allianz morali yao ikiwa juu baada ya ushindi wa dakika za majeruhi walioupata wikendi iliyopita dhidi ya Wolfsburg – Shukrani kwa magoli ya Paco Alcacer dakika ya 90 na 94, Bayern Munich na Borussia Dortmund watakuwa wanakutana kwa mara ya mia moja Jumamosi hii na katika kuadhimisha uhasimu wao watabadilishana rangi za sare zao, Bayern wakivaa sare za njano huku Dortmund wakivaa sare nyekundu.
Ukimuuliza Mwinyi Zahera ishu za Ajib kurudi Simba SC….