Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi (Kamati Ya Saa 72) inayoendeshwa na bodi ya ligi nchini imefanya maamuzi baada ya kupitia na kujadili ripoti ya michezo ya mzunguuko wa kwanza na wa pili ya ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2018/19 iliyoanza rasmi August 22 2018
Kamati hiyo iliyokutana mwishoni mwa wiki iliyopita imewachukuliaa hatua za kinidhamu baadhi ya waamuzi waliokua wamesimamishwa na kamati ya waamuzi ya shirikisho la soka Tanzania TFF, kufuatia kushindwa kuzimudu sheria 17 za mchezo wa soka.
Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya ligi Boniface Wambura amezungumza na waandishi wa habari na kuweka wazi maamuzi hayo
Maamuzi ya TFF na Simba kwa wachezaji 6 waliondolewa Taifa Stars