Moja kati ya wachezaji ambao majina yao yamekuwa makubwa sana kwa siku za hivi karibuni ni pamoja na Matthijs de Ligt wa Ajax ya Uholanzi, hiyo inatokana na uwezo wake aliouonesha katika michezo ya UEFA Champions League akiwa na timu yake ya Ajax ambayo ilifika hadi hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Kutokana na uwezo wake aliounoesha De Ligt kwa sasa anawaniwa na vilabu mbalimbali vikubwa vya soka barani Ulaya, huku wengi wakimtaja kama chaguo la kwanza la makocha wengi licha ya kuwa De Ligt kuwa na umri wa miaka 19, Man United walikataa kumsajili mchezaji huyo kwa madai ya kuhofia kuwa ataongezeka uzito kutokana na familia yake kuwa asili ya unene.
Man United bado wanahusishwa kumuhitaji mchezaji huyo, Juventus ya Italia pamoja na FC Barcelona ambao wanatajwa kuwa wao wameshafikia makubaliano na Ajax ya kumsajili mchezaji huyo kwa dau la pound milioni 60, hata hivyo usajili ya De Ligt unaweza kuwa mgumu kwenda club yoyote kutokana na wakala wake Mino Raiola ambaye lazima ahusike kwenye usajili kufungiwa na FIFA kwa miezi mitatu.
Samatta kaweka historia Ubelgiji, mchezaji wa tatu kuwahi kushinda Ebony Award 2019