Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta jina lake limerudi kwenye headlines baada ya kufanikiwa kuikomboa timu yake ya KRC Genk katika mchezo wa play offs Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya KAA Gent.
Mbwana Samatta leo ameichezea KRC Genk kwa dakika 36 akitokea benchi dakika ya 54 kuchukua nafasi ya mgiriki Nikolaos Karelis timu yao ikiwa nyuma kwa goli 1-0 wakati huo, dakika 12 baada ya Samatta kuingia akafanikiwa kuisawazishi KRC Genk goli na kuufanya mchezo kumalizika kwa kufungana goli 1-1.
Goli la KAA Gent lilifungwa na dakika ya 15 na Yuya Kubo , Mbwana Samatta ambaye alikuwa majeruhi kwa kipindi cha miezi miwili leo anafanikiwa kufunga goli lake la kwanza na Genk kwa mwaka 2017 lakini ni goli lake la kwanza kufunga baada ya kuichezea Genk michezo 19 kwa dakika 1015.
Mara ya mwisho Mbwana Samatta kuifungia goli KRC Genk kabla ya leo ikuwa October 25 2017 katika mchezo dhidi ya Club Brugge, ambapo Genk walipata ushindi wa magoli 2-0, ambapo Samatta alifunga goli la pili dakika ya 90.
Genk sasa wapo nafasi ya sita katika timu 6 zinazocheza game za Play offs Ligi Kuu Ubelgiji kwa ajili ya kuwania nafasi ya kucheza michuano ya UEFA Champions League na Europa League msimu wa 2018/2019 Genk wakiwa na point 32 na wamesalia na michezo miwili ili wapate nafasi ni lazima wamalize nafasi ya nne.
Simba kama Man City tu wametwaa Ubingwa wa Ligi nje ya uwanja leo