Waziri wa afya na Maendeleo ya Jamii Ummy Mwalimu hatimae amefanikiwa kuzindua chama cha urembo na vipodozi Tanzania (TCA), chama ambacho kinalenga kuwakutanisha pamoja watu wa tasnia ya urembo ili kutatua changamoto na kuendeleza tasnia ya urembo nchini.
Tasnia ya urembo ni miongoni mwa tasnia zinazokuwa zaidi duniani na hadi kufikia 2017 tasnia ya urembo ilikuwa na thamani ya dola Bilioni 532 duniani kote, huku ikitegemewa kufikia thamani ya dola bilioni 863 itakapofikia mwaka 2024.
Pamoja na kuwa na ukubwa huo lakini nchi za Afrika ikiwemo Tanzania zimekuwa zikifaidika ama kufikia asilimia tatu tu ya soko hilo, hivyo chama hicho kinalenga kukuza tasnia ya urembo kufikia soko la dunia nzima kwa kiasi kikubwa na kupambania maslahi mapana ya tasnia hiyo.
WANAFUNZI WA MASOMO YA FIZIKIA KWENYE UTHUBUTU WA KUTATUA MATATIZO KITEKNOLOJIA