Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi anayeichezea Stoke City ya England Saido Berahino amekumbana na adhabu nchini England, kutokana na kukutwa na hatia kuhusiana na kesi yake ya kuendesha gari nchini England akiwa ameelewa.
Berahino mwenye umri wa miaka 25 mara kadhaa amewahi kutuhumiwa kuwa anaendesha gari akiwa ameelewa lakini kosa alilohukumiwa nalo ni kosa la kuendesha gari yake aina ya Range Rover akiwa amelewa February 18 nchini England, Berahino ambaye anasubiriwa nchini kwao Burundi kwa ajili ya michuano ya AFCON 2019 itakayochezwa Misri amepewa adhabu mbili.
Mahakama ya Highbury imemuhukumu Saido Berahino adhabu ya kutoendesha gari kwa miezi 30 pamoja na kumpiga faini ya pound 75000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 220, Berahino ni mchezaji wa timu ya taifa ya Burundi aliyekulia katika academy ya West Bromwich Albion na amewahi kucheza timu za taifa za vijana za England katika ngazi zote ila kukosa nafasi timu ya wakubwa kukamfanya akumbuke taifa lake 2018.
Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC