Winga wa FC Bayern Munich ya Ujerumani Kingsley Coman amezichukua headlines kufuatia kauli yake nzito aliyoitoa akiwa bado ana umri wa miaka 22, Coman ameeleza msimamo wake kuwa hayuko tayari kuona tena anafanyiwa upasuaji mkubwa kama atapata majeruhi katika soka.
Hivyo ameamua kuweka wazi ikitokea akapata jeraha kubwa katika soka tena litakalohitaji upasuaji basi ataacha kucheza soka na kutafuta maisha kwa njia nyingine, Coman amerudi uwanjani mwezi huu toka alipoumia enka mapema mwanzo wa msimu.
Coman aliumia enka ya mguu wake wa kushoto wakati wa game ya ufunguzi wa msimu kati ya FC Bayern dhidi ya Hoffenheim ambayo ilikuwa ni game yake ya kwanza kucheza toka alipocheza game ya mwisho mwezi February na kuumia enka hiyo hiyo ya mguu wa kushoto na amekosekana katika fainali za Kombe la Dunia na taifa lake la Ufaransa.
“Nimekuwa na msimu mgumu sana na nimekuwa nikiumia nilikuwa naona kama mwisho wa dunia kwangu mimi, namatumaini sitapitia tena katika wakati nilipitia, kiukweli inatosha sitokubali upasuaji wa tatu, hiyo itaashiria kuwa mguu wangu haujatengenezwa kwa kiwango hiki na nitatafuta maisha kwa njia nyingine”>>> Coman
MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe