Jumamosi ya July 22 2017 mtanzania Mbwana Samatta alipata nafasi ya kuiongoza safu ya ushambuliaji ya timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Everton FC inayodhaminiwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.
Mchezo wa Everton dhidi ya KRC Genk uliyochezwa nchini Ubelgiji katika uwanja wa Luminus Arena, umempa nafasi nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta kuonesha uwezo wake dhidi ya Everton ambayo ni miongoni mwa vilabu saba England ambavyo havijawahi kushuka daraja toka kuanzishwa kwa mfumo wa Ligi Kuu England 1992.
Mbwana Samatta ambaye ndio mshambuliaji tegemeo wa KRC Genk baada ya kuumia kwa mgiriki Nikolaos Karelis aliifungia KRC Genk goli la kusawazisha dakika ya 55, hiyo ni baada ya Wayne Rooney kuifungia Everton goli la kwanza dakika ya 45 kwa kutumia vyema assist ya Sandro Ramirez.
Goli la @samatta77 aliloisawazishia KRC Genk katika sare ya 1-1 game ya kirafiki vs Everton leo #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/MCOUnYXtMj
— millard ayo (@millardayo) July 22, 2017
Sandro assist ?
Rooney goal ?@WayneRooney puts #EFC ahead! 1-0#EvertonLive: https://t.co/m1rIpwvD9C pic.twitter.com/DOMiSZlVF4
— Everton (@Everton) July 22, 2017
VIDEO: Gor Mahia vs Everton: Full Time 1-2 (ALL GOALS JULY 13, 2017)