Baada ya vuguvugu la muda mrefu hatimae jioni ya October 8 2018 club ya Simba SC imetangaza kuachana rasmi na kocha wao msaidizi raia wa Burundi Irambona Masoud Djuma kwa maslahi mapana ya club hiyo.
Simba SC kupitia afisa habari wao Haji Manara wametangaza kufikia makubaliabo ya kuvunja mkataba na kocha huo, sababu ikitajwa kuwa ni maslahi mapana ya club “Kwa niaba ya uongozi wa Simba SC ningependa kwa masikitiko nitangaze rasmi kwamba club ya Simba na kocha wetu msaidizi Masoud Djuma tumesitisha mkataba wetu kiungwana wa yeye kuendelea kuwa kocha wa Simba”>>>Manara
Baada ya Manara kutangaza hivyo kocha Masoud Djuma alikuwa nayo ya kuongea kwa wana Simba SC “Walinipa fursa ya kufika Simba sikuwa najua kama nitafika Simba leo Mungu amenijalia nimefika Simba, watu wengine wa kushukuru zaidi ni watu wangu wa Simba na mashabiki, kazi ilikuwa inafanyika lakini tulipofikia kila jambo lina mwanzo na mwisho”>>>Masoud Djuma
Kocha msaidizi Simba SC Masoud Djuma baada ya kusitishiwa mkataba wake leo hii na Simba SC #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/k6IxrCJOrB
— millardayo (@millardayo) October 8, 2018
RASMI: Club ya Simba SC leo kupitia kwa afisa habari wao @hajismanara imetangaza kuachana na kocha wao msaidizi raia wa Burundi Irambona Masoud Djuma kwa maslahi mapana na club hiyo #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/EYkULAX7kj
— millardayo (@millardayo) October 8, 2018
“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga