Jina la golikipa wa Besiktas ya Uturuki lilitawala sana vichwa vya habari msimu uliopita akiwa Liverpool baada ya mchezo wa fainali ya UEFA Champions League kati ya Liverpool dhidi ya Real Madrid ambao ulimalizika kwa Liverpool kupoteza na Karius kuonekana mnyonge dhidi ya ufundi wa Gareth Bale.
Leo tena Karius akiichezea Besiktas ya Uturuki katika game ya UEFA Europa League dhidi ya KRC Genk ya Ubelgiji inayochezewa na mtanzania Mbwana Sambatta, Karius amekutana tena na umahiri na ufundi wa Samatta.
Samatta katika game ya tatu ya Europa leo ameisadia timu yake ya KRC Genk kupata ushindi wa magoli 4-2, Mbwana Samatta akihusika katika upatikanaji wa magoli matatu kati ya hayo akifunga magoli mawili dakika ya 23 na 70 na kutoa pasi ya goli.
Goli la tatu la KRC Genk lilifungwa na Ndongala dakika ya 81 la nne na Piotrowski dakika ya 83 wakati magoli pekee ya Besiktas yalifungwa na Vagnar Love dakika ya 74 na 86, ushindi huo sasa unaifanya Genk kuongoza Kundi I kwa kuwa na point sita wakipoteza mchezo mmoja nafasi ya pili ikifuatiwa na Sarsborg 08 wenye point nne.
Samatta anazidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania tuzo ya ufungaji bora wa michuano hiyo, kwani amefunga jumla ya magoli matatu hatua ya makundi akiwa na wastani wa kufunga goli moja kila mechi lakini katika list ya wanaoongoza kwa ufungaji magoli mengi yupo nafasi ya pili akifungana na wachezaji wengine wanne, Munas Dabbur wa RB Salzburg akiongoza kwa kuwa na magoli matano.
“Tumeshinda ili kuweka tabasamu usoni kwa MO Dewji”-Kocha Simba SC