Kama ulikuja Dar es Salaam miaka kumi iliyopita na ukirudi kwasasa basi lazima ukute mabadiliko makubwa yaliyofanywa katika Sekta mbalimbali kuanzia Barabara, Majengo na mengineyo.
Ukiacha uboreshwaji uliofanywa kwenye sekta mbalimbali kingine ambacho kimenivutia ambacho huenda utapendezwa nacho.
Ni Kwamba Tips wamefanya mapinduzi makubwa na kutoa ajira katika sekta ya viota vinavyowakutanisha watu mbalimbali ukiacha ile Tips Mikocheni aliyoifungua Mwaka 2017 sasa kwa Mwaka huu 2022 wametumia Fursa na kufungua chimbo lingine lenye utofauti liitwalo Tips Coco Beach lililopo Oysterbay Dar es Salaam.
Tips wanastahili pongezi na wameweza kuwa wa kitofauti na maeneo mengine ya Dar kwa huduma zao pamoja kwa ubunifu walioufanya wa kuamua kuiteka Jumatatu ambayo wengi tumezoea ni siku ya kazi lakini wao wamekuja na kitu cha tofauti.
Akizungumza na millardayo.com & Ayo TV msemaji wa Tips alisema…’Kwanza tunawashukuru Millardayo.com kwa kuendelea kuwa nasi siku zote pili wadau wetu ambao wamekuwa bega kwa bega nasi, habari njema ambayo ninataka kuwajuza ni kwamba kwasasa tumefungua eneo jingine lipo Oysterbay tumelipa jina la Tips Coco Beach”- Msemaji
Kwa mujibu wa miongoni mwa wamiliki alisema eneo hili linauwezo wa kuingia watu wasiopungua mia 500 ambao wataweza kuhudumiwa na kufurahi huduma inayotolewa.
“lengo letu ni kuhakikisha wadau wanafurahi na kuburudika hivyo Uongozi tulikaa na kuchagua siku ya Jumatatu kuwa siku ya kuwaleta wasanii wakubwa hata Ma Dj’s kwaajili ya kutoa uchovu kwa wateja wetu waliotoka maofisini hata katika biashara zao za kila siku”– Msemaji wa Tips
“Hivyo Tips Coco itakuwa ikiandaa shughuli kila Jumatatu na hakutakuwa na kiingilio chochote bali ni bure ili mdau wetu anapofika atahudumiwa na kumdhihirishia kwamba Jumatatu sio siku ya kurudi nyumbani bali anaweza kuja katika eneo letu akapata burudani tulizoziandaa”– Msemaji wa Tips
“Na Octoba 10, 2022 tutakuwa na Ma Dj’s Finomol ambao wataungana na Ma Dj’s wetu kuhakikisha Jumatatu inageuzwa na kuwa Ijumaa haijawahi kutokea nawakaribisha wadau wote”- Msemaji wa Tips
“Mwisho tunakaribisha mawazo kwa wasanii wetu wa ndani kwani ni fursa maeneo ya wazi kama haya ili waweze kukutana na mashabiki zao”– Msemaji wa Tips