Timu ya taifa ya Burundi kwa mara ya kwanza katika historia leo imefanikiwa kuweka rekodi mpya katika soka lake baada ya kutinga fainali za mataifa ya Afrika AFCON 2019 zitakazofanyika nchini Misri June 2019, hivyo imefanikiwa kuweka rekodi kwa mara ya kwanza Afrika Mashariki inaingiza mataifa matatu (Kenya, Burundi na Uganda) katika fainali za AFCON huku Tanzania ikiwa na matumaini.
Burundi imefuzu kucheza michuano hiyo kwa mara ya kwanza huku ikimuacha staa wa Arsenal Pierre Emerick Aubameyang kichwa chini kutokana na taifa lake kutolewa, hiyo ni baada ya mchezo wao wa leo kumalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1.
Golikipa aliyesimama katika lango la Burundi kuokoa michono ya Aubameyang aliyekuwa hatari kiasi cha kuifungia Gabon goli moja, golikipa wa club ya KMC ya Tanzania Jonathan Nahimana hivyo anakuwa sehemu ya historia ya kuipeleka Burundi katika fainali za AFCON kwa mara ya kwanza.
Mataifa mengine 19 ambayo tayari yamefuzu ni Angola, Madagascar, Tunisia, Misri, Senegal, Uganda, Nigeria, Mali, Morocco, Algeria, Ivory Coast, Mauritania, Guinea, Burundi, Kenya, Ghana, Guinea Bissau, Namibia na Cameroon huku Tanzania ikiombea ushindi kesho dhidi ya Uganda na kuombea Lesotho afungwe na Cape Verde.
Mashabiki wa Simba na Yanga waiongelea Simba VS AS Vita hapo kesho !!