Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Tulia Ackson leo amefanya mkutano na waandishi wa habari kupitia taasisi yake Tulia Trust na kuzinduzia rasmi tamasha lake la ngoma za asili linalofahamika kama Tulia Trust Traditional Dance.
Dr Tulia ameeleza maboresho waliyoyafanya katika tamasha la Tulia Trust Traditional ni pamoja na kuongeza idadi ya vikundi vya ushiriki, kutoka kushirikisha baadhi ya mikoa hadi sasa itakuwa inashirikisha Tanzania nzima.
“Tulia Trust tunapenda kuwafahamisha dunia nzima lile tamasha letu linalofanyika kila mwaka limekaribia kama tulivyosema mwaka huu itashirikisha Tanzania nzima hadi Zanzibar kwa hiyo tuko tayari kwa hilo zoezi litakalofanyika kuanzia September 20 hadi September 22”
“Tamasha hili huwa tunafanyia ambapo huwa wilayani Rungwe mjini Tukuyu jijini Mbeya na tupo kwa ajili ya kuwakumbusha watanzania na kuuenzi utamaduni wetu na tungependa pia dunia ijue utamadunia wetu, mwaka huu tutakuwa na vikundi 108”
Haji Manara kaeleza sababu za kuwasajili Wawa, Dida na Kagere