Baada ya kudaiwa kuwepo na tatizo la kifedha ndani ya club ya Dar es Salaam Young Africans, aliyekuwa kocha wao msaidizi Shadrack Nsajigwa ameachana na club hiyo.
Shadrack Nsajigwa ameachana na club ya Yanga kwa kile kinachoelezwa kuwa ni mkataba wake kumalizika na club hiyo kumalizika.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Shadrack Nsajigwa aliwahi kuichezea club ya Dar es Salaam Young Africans na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars akiwa kama nahodha kabla ya kuamua kustaafu na kuanza kazi ya ukocha.
AyoTV ilivyomnasa staa wa zamani wa Liverpool Airport KIA