Taarifa zilizoripotiwa kutokea nchini Ureno kuhusiana na golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania na club ya Real Madrid Iker Casillas ni kuwa amelazimika kukimbizwa hospitali ghafla akiwa mazoezini baada ya kuugua ghafla.
Casillas akiwa na katika mazoezi na timu yake ya FC Porto ya nchini Ureno, alipata matatizo ya mshituko wa moyo na kulazimika kukimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa huduma zaidi, kwani ugonjwa wa mshituko wa moyo umekuwa hatari zaidi kwa wachezaji kiasi cha kupelekea baadhi ya kupoteza maisha.
Baada ya kukimbizwa hospitalini ni kuwa Iker Casillas ambaye alitumiwwa jumbe za faraja na wachezaji mbalimbali wakiwemo aliocheza nao Real Madrid kama Gareth Bale na Sergio Ramos, kwa sasa anaendelea vizuri na hali yake imeimarika, Casillas mwenye umri wa miaka 37 alijiunga na FC Porto 2015 baada ya kuichezea Real Madrid kwa miaka zaidi ya 15.
Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania