Makumi ya watu waliuawa katika mapigano makali wakati wa mechi ya soka nchini Guinea Jumapili jioni.
Vurugu hizo zilitokea wakati wa mechi kati ya timu ya soka ya Labe na Nzerekore huko Nzerekore, jiji la pili kwa ukubwa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi
Wakati idadi kamili ya vifo bado haijafahamika, vyanzo vya hospitali vya ndani viliripoti “maafa kadhaa.” Daktari mmoja katika eneo la tukio alikadiria kuwa idadi ya waliofariki inaweza kuwa “karibu 100.”
Waziri Mkuu wa Guinea Bah Oury alilaani ghasia hizo katika taarifa kwenye X.
“Serikali inajutia matukio ambayo yaliharibu mechi ya soka kati ya timu za Labe na Nzerekore leo mchana huko Nzerekore,” alisema.
“Serikali inafuatilia kwa karibu hali hiyo na inasisitiza wito wake wa utulivu ili huduma za hospitali zisikwamishwe katika kutoa huduma ya kwanza kwa majeruhi.”
Taarifa zaidi zitatolewa kadri zitakavyopatikana, aliongeza
Kulingana na ripoti hiyo, maamuzi ya waamuzi ambayo yaliwafanya wachezaji wawili wa Labe kupokea kadi nyekundu na kufuatiwa na adhabu dhidi ya timu hiyo hiyo yalizua vurugu.