Utawala wa kijeshi nchini Guinea umeagiza kufunwa kwa akaunti za benki na kutwaliwa kwa pasipoti za wajumbe wa serikali baada ya kuivunja serikali kwa sababu ambazo bado hazijajulikana.
Siku ya Jumatatu wanajeshi ambao walichukua madaraka kwa nguvu mnamo mwezi Septemba 2021 walitangaza kuvunjwa kwa serikali ambayo walikuwa wameiweka mnamo mwezi Julai 2022.
Wameamua kufungia akaunti za wajumbe wa serikali, kuchukua hati zao zote za kusafiri, pamoja na magari yote ya kazi, na kuwany’anganya walinzi wao na wasaidizi wao, inabaini taarifa iliyosomwa siku ya Jumatatu jioni kwenye runinga ya serikali na Jenerali Ibrahima Sory Bangoura, mkuu wa majeshi, mbele ya askari wengine ishirini.
Hakuna maelezo ambayo yametolewa hadharani kwa hatua hizi, wala kwa kuvunjwa kwa serikali. Watawala wa Guinea, kama wale ambao wamejidhihirisha katika nchi kadhaa za Afrika Magharibi tangu 2020, wamefanya vita dhidi ya ufisadi kuwa moja ya maneno yake.