Rais wa mpito wa Guinea Kanali Mamadi Doumbouya, ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa, kufuatia ajali ya moto iliyotokea katika ghala kubwa la mafuta usiku wa jumapili mjini Conakry, na kusababisha vifo vya watu 18 na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa.
Akihutubia kwa njia ya televisheni, Rais Doumbouya ametangaza kuwa kwenye kipindi cha maombolezo ya kitaifa, bendera ya Guinea itapepea nusu mlingoti kote nchini humo na katika ofisi na balozi zake nje ya nchi
Moto ulilipuka katika kiwanda cha mafuta ya petrol muda mfupi baada ya mlipuko mkubwa kutokea usiku wa jumapili , ofisi ya rais wa Guinea imesema katika taarifa yake.
Eneo hilo lililoko katika wilaya ya Kaloum ina maofisi mengi ya serikali.
Haikuelezwa wazi nini kimesababisha moto huo katika kiwanda ambapo kinasambaza mafuta kwenye maeneo mengi ya Guinea, hali iliyozusha hofu ya kuvurugika kwa usambazaji mkubwa.
Maafisa hawajathibitisha idadi ya majeruhi ingawa vyombo vya habari vya ndani viliripoti kuwa maelfu ya watu wamejeruhiwa wengi wao wamelazwa hospitali wakiwa na majeraha mabaya.