Wakati wito wa kumtaka ajiondoe kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Ikulu ya White House kwa sababu za kiafya ukiongezeka, Joe Biden alianza vibaya mkutano wake na waandishi wa habari Alhamisi jioni, kipindi kilichokua kinasubiriwa na watu wengi.
Joe Biden alianza kwa kuwa na wasiwasi kwa kujichanganya, kabla ya kuchanganya, majina ya viongozi wawili wanaopambana katika vita kwa sasa.
nakumwita Volodymyr Zelensky kwa jina la adui yake.
Rais wa Marekani, Joe Biden ametambulisha kimakosa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy kama ‘Rais Putin’ “katika mkutano wa NATO unaofanyika jijini Washington kabla ya kujirekebisha mwenyewe akisema “Nimemakinika sana kuhusu kumpiga Putin.”
Kisha kuchanganya majina tena la makamu wake wa rais na mpinzani wake wa chama cha Republican Donald Trump.
Alisema Kamala Harris ndilo jina ambalo limetajwa na kupendekezwa mara nyingi kuchukua nafasi yake ikiwa ataachana na kinyang’anyiro cha kuwania Ikulu ya White House. “Anaweza kupambana,” Joe Biden amesema.
“Singeweze kumchagua ikiwa sikufikiria angeweza kuwa rais. Tangu mwanzo. Sikuficha hili. Ana sifa za kuwa rais. Ndiyo maana nilimchagua.”
Joe Biden amerudia mara kadhaa kwamba anataka “kumaliza kazi” iliyoanza mnamo mwaka 2020, na amehakikisha kwamba bado ataweza, ikiwa atachaguliwa tena, “kusimamia” marais wa China na Urusi, Xi Jinping na Vladimir Putin, katika kipindi cha miaka mitatu .
“Nilifanyiwa vipimowa hali ya juu wa mishipa ya fahamu mara tatu” uliofanywa na daktari wa neva, vipimo vya mwisho nilivifanya “mwezi Februari,” amekumbusha, na “wanasema nina hali nzuri.” Kwa mara nyingine tena alifuta uchnguzi mbaya wa kura ya maoni.