Tukio hilo la kukata umeme lilifanyika katika jimbo la India la Bihar katika kijiji kizima wenzi hao waweze kukutana na mvulana huyo alitoka kutoka cha jirani bila mtu yeyote kuwaona pamoja wakati huo.
Watu wa Bettiah, katika wilaya ya Champaran Magharibi ya Bihar, walikuwa wamekaa kwa zaidi ya wiki moja wakishuhudia jambo hilo likijiridia kutokana na hitilafu zisizo za kawaida za umeme ambazo zilionekana kutokea karibu kila usiku.
Na wakati wa giza totoro ilikuwa ni fursa nzuri kwa wezi, hivyo watu walitoa wito kwa kampuni ya umeme kurekebisha mtandao wao, lakini wawakilishi wake hawakuripoti masuala ya miundombinu.
Hakuna aliyeweza kuelewa kilichokuwa kikiendelea hadi usiku mmoja, wakati baadhi ya wenyeji waliposimama kukesha katika kijiji hicho na kuwakamata wenzi hao walipokutana gizani nakufanya walivyo zoea kila mara ndipo ilipobainika kuwa msichana wa eneo hilo, Priti Kumari, alikuwa amependana na Rajkumar, kijana kutoka kijiji pinzani cha jirani, ambao walikata nguvu ya umeme iliwakutane.
mwishowe, ili kuepusha vurugu zaidi na kukatika kwa umeme, watu wa vijiji hivyo viwili waliamua kwamba wanandoa hao wachanga wafunge ndoa, hivyo harusi yao ikafanywa rasmi katika hekalu la mahali hapo.