Naibu Waziri wa Afya Tanzania Dr. Godwin Mollel amesema mwitikio wa Watanzania kutaka kupata chanjo ya corona ni mkubwa na hadi sasa ni zaidi ya Watanzania milioni moja wamewasilisha maombi ya kuchanjwa.
“Mpaka sasa Wizara ya Afya kwa maombi ya Watu wanaotaka chanjo ni zaidi ya Milioni moja, nafikiri inapelekea meseji kwamba watu wanaoogopa chanjo ni perception ya mtu na mtu” Naibu Waziri wizara ya Afya, Dr. Godwin Mollel
“Sisi wizara ya Afya yeyote anayepinga kuhusu chanjo kama Mbunge,Askofu Gwajima kwangu mimi kama mtu wa wizara ya afya namuona kama client wangu ana mambo yake ambayo yanayohusu usalama wake, kwahiyo najiona kwa sehemu yangu natakiwa kufanya kazi zaidi ya kumfundisha, kuelimisha” Naibu Waziri wa Afya, Dr. Mollel.
“Kuna mgonjwa anakuja hospitali analetwa na ndugu unamwambia anywe dawa anakataa, huwezi kumwambia kwa ukali yeye ni mjinga na aondoke hapana, ni kuhakikisha napambana naye hadi akubali kwa hiari yake, akipata dawa akipona wengi wanarudi kushukuru ndio kama hawa wanaopinga chanjo” Dkt. Mollel