Mshambuliaji nguli wa Arsenal, Thierry Henry anaripotiwa kuwa yuko mbioni kuinoa klabu ya Ufaransa ya Paris Saint-Germaine, PSG na anatazamiwa kuchukua nafasi ya meneja msaidizi katika klabu ya PSG iwapo klabu hiyo itamtaja Julian Nagelsmann kama meneja anayefuata.
Galtier anatarajiwa kuacha nafasi yake ya ukocha katika klabu hiyo ya mji mkuu licha ya kuiongoza PSG kutwaa ubingwa wa Ligue 1 katika msimu uliomalizika hivi punde.
Huku Galtier akiwa tayari kuondoka, L’Equipe inasema kocha wa zamani wa Bayern Munich Nagelsmann atatajwa kuchukua nafasi yake na Mjerumani huyo anataka kumuongeza Henry kama msaidizi wake.
Mabingwa hao wa Ligue 1 wako kwenye mazungumzo na meneja wa zamani wa Bayern Munich, Julian Nagelsmann, kuchukua nafasi ya Christophe Galtier kama kocha, ESPN inaripoti.
Nagelsmann anatarajiwa kuwa mjini Paris siku ya Jumanne kwa mazungumzo.
PSG wamemfanya kuwa mlengwa wao mkuu, huku kocha huyo Mjerumani akitaka Thierry Henry ajiunge naye kama msaidizi wake.
Wanamwona Nagelsmann kama meneja bora wa kutumia mazao yenye vipaji ya wachezaji wachanga wanaokuja.
Galtier anatarajiwa kutimuliwa PSG baada ya kuifundisha kwa msimu mmoja pekee licha ya kuiongoza klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligue 1.
Muda wake wa utumishi ulishuhudia klabu hiyo ikipata hasara ya kuondoshwa katika hatua ya 16 bora katika Ligi ya Mabingwa.