Imepita siku moja baada ya taarifa kutoka nchini Marekani kuonesha kuwa wanafunzi 17 wa shule ya sekondari Marjory Stoneman Douglas High School iliyoko Parkland, Florida kuuawa kwa kupigwa risasi na mwanafunzi mwenzao.
Kutokana na hilo Chama cha Democrats nchini humo kimeshusha lawana za shambulio hilo kwa Rais Donald Trump na Spika wa Bunge la nchi hiyo Paul Ryan kwa kukataa kuruhusu mjadala wa sheria ya kumiliki silaha.
Kumekuwa na mijadala mbalimbali ya wanaharakati ambao wamekuwa wakishinikiza kufanyika kwa mabadiliko ya sheria ya umiliki wa silaha za moto kwa wananchi wa nchi hiyo ili kupunguza matukio ya mauaji ya silaha hizo.
Maelfu ya waombolezaji wamekutana Florida katika eneo hilo la shule ili kuwasha mishumaa na kufanya ibada ya kuwakumbuka watu hao 17 waliopoteza maisha kutokana na shambulio hilo siku ya jana
Agizo la Dr. Mwigulu kwa IGP Sirro kuhusu Kiongozi wa CHADEMA aliyeuwawa