Mwili wa Bi. Linah George Mwakyembe mke wa Waziri wa Habari Dr. Harrison Mwakyembe utaagwa leo ambapo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan atawaongoza waombolezaji kuuaga mwili huo Kunduchi, DSM.
Gumzo la fedha za ESCROW limechukua sura mpya baada ya TRA kutozitambua zaidi ya Tsh. 40 Milioni ambazo zilirudishwa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja pamoja na issue nyingine ambazo tayari nimekusogezea karibu kupitia millardayo.com.
Baada ya Necta kutangaza matokeo, Shule ya Sekondari Njombe imelalamika ikidai matokeo hayo hayaendani na wastani wake wa ufaulu. #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Siku moja baada ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Lowassa kusema atagombea Urais 2020, @ccm_tanzania imesema itamshinda tena. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
CHADEMA imeitaka Jumuiya ya Kimataifa kuacha kuifadhili Tanzania kwa madai kuwa kuna ukiukwaji wa demokrasia na haki za binadamu #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Wafanyabiashara zaidi ya 200 waliokuwa wanafanya biashara Mailimoja, Pwani wameomba msaada wa Rais JPM waendelee kufanya biashara. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Serikali wakati wowote kuanzia sasa itaanza kulipa malimbikizo ya madai ya watumishi wakiwemo wastaafu, kupandisha vyeo wenye sifa. #Nipashe
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Upelelezi kesi ya kutakatisha fedha inayowakabili Rais wa TFF na wenzake haujakamilika hivyo kesi imesogezwa mbele hadi July 31. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Lissu amesema anazo taarifa za Waziri Mkuu wa zamani E. Lowassa kufikishwa Mahakamani wakati wowote. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
TRA imesema haizitambui zaidi ya Tsh. 40 milioni zilizoingizwa kwenye akaunti yake wiki moja iliyopita na William Ngeleja. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Baadhi ya Madiwani wa CHADEMA wa H'shauri ya Meru waliojiuzulu hivi karibuni wameomba kazi ya kujitolea H'shauri Arusha Vijijini. #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Polisi Mwanza inamshikilia mwalimu wa Shule ya Msingi Mabomba, wilayani Kwimba akidaiwa kufanya mapenzi na mwanafunzi wa Form 4. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Waziri wa Mazingira @JMakamba amewasimamisha kazi watumishi wa NEMC kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili ikiwemo rushwa. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Mtu mmoja Dodoma ambaye alidaiwa kufariki na kuzikwa ameibuka wakati ndugu na jamaa zake wakiwa katika maombolezo ya msiba wake. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
"Wanasiasa wanajua sheria ya vyama vya siasa inasemaje, lakini wanashindwa kuifuata." – Jaji Francis Mutungi. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Msajili wa Vyama vya Siasa amesema hana mamlaka ya kutoa vibali vya mikutano ya ndani au nje na maandamano kwa vyama vya siasa. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
DC Nkasi amepiga marufuku kwa baadhi ya watumishi wa afya kuwachangisha wananchi fedha za kununulia mafuta ya gari la wagonjwa. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Watoto wanne wamekufa kwa kukosa hewa baada ya kujifungia kwenye gari moja kuanzia asubuhi hadi usiku maeneo ya Jang'ombe, Unguja #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Jeshi la Polisi Tarime-Rorya linawashikilia watu wawili wakidaiwa kumkata mkono Mkaguzi wa Polisi wakati wakigombea mwanamke. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Mbunge wa Mwanga Prof. Maghembe amewaasa Wabunge kuepuka kupanga safu ktk uongozi wa chama ngazi ya Jimbo kuepuka kukidhoofisha. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Mikoa 13 imekamilisha kazi ya kuorodhesha Kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara 2017/18. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Serikali imeahidi kuzidisha mapambano dhidi ya rushwa, ukiritimba ktk mamlaka zinazohusiana na uwekezaji ili kuvutia wawekezaji. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Imeelezwa kuwa mwaka wa fedha 2017/18 mishahara ya Watumishi wa Umma italipwa kupitia BoT kwenda ktk akaunti za Watumishi wa Umma #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Baadhi ya viongozi wa dini wamebariki hatua ya Serikali kufuatilia na kufungia vituo vya mafuta vilivyokaidi agizo la kutumia EFD #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Wahamiaji haramu 66 kutoka Ethiopia ambao walifungwa ktk magereza mkoani Pwani wamerudishwa kwao baada ya kusamehewa na Rais JPM. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Wahitimu wa Vyuo vya Elimu ya Juu wametakiwa kuitumia elimu waliyoipata katika kufanya ujasiriamali badala ya kufikiria kuajiriwa. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo anatarajia kuwaongoza Watanzania kuuaga mwili wa aliyekuwa mke wa Waziri Dr. Mwakyembe. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Waumini wawili wa Kanisa la Siloamu la Manda Kilesi, kijijini Keni, wamefariki dunia wakati wakibatizwa ktk Mto Ugwasi, Rombo, KLM. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Polisi DSM imeanza operesheni maalumu kuwasaka wahalifu wanaojihusisha na wizi wa vifaa vya magari katika maeneo mbalimbali ya DSM. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Rais JPM atafungua na kuzindua miradi 9 ya barabara na uwanja wa ndege Kagera, Kigoma, Tabora na Singida kati ya July 19-25. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Vyama vya upinzani vimetakiwa kupongeza juhudi za maendeleo zinazofanywa na Rais JPM katika kupigania rasilimali za Watanzania. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 18, 2017
Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu amekutana na Wanahabari DSM na kuzungumzia issue mbalimbali ikiwemo tukio la kukamatwa kwa Katibu Mkuu wa chama hicho Dr. Vincent Mashinji na Edward Lowassa kupelekwa Mahakamani…PLAY kwenye VIDEO hii kutazama kila kitu.