Leo October 2, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo inayomkabili mfanyabiashara Yusuf Ali maarufu kama ‘Mpemba wa Magufuli’ na wenzake watano hadi October 17, 2017.
Hatua hiyo inatokana na wakili wa Serikali, Elia Athanas kumueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, kuwa jalada la kesi hiyo bado kwa Mkurugenzi wa mashtaka (DPP), hivyo anaomba iahirishwe hadi tarehe nyingine.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Charles Mrutu, mkazi wa Mlimba, Morogoro, Benedict Kungwa, mkazi wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima, mkazi wa Mbezi, Ahmed Nyagongo, dereva na Pius Kulagwa, ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka manne ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 785.6.
Ulipitwa na hii? Saa 96 baada ya kuachiwa huru, Manji karudi Mahakamani leo