January 30, 2018 stori kubwa ilikuwa inatokea +254 Kenya kuhusu ishu ya kuapishwa kwa Raila Odinga, sasa Leo January 31, 2018 habari kutoka Kenya ni kwamba Jeshi la Polisi nchi humo limemtia mbaroni Mbunge wa Ruaraka, Tom J Kajwang’, ambaye alisimamia zoezi la ‘kuapishwa’ kwa Kiongozi wa Muungano wa Upinzani (NASA) Odinga.
Mbunge huyo amekamatwa Jijini Nairobi akiwa katika viwanja vya Mahakama Kuu kusikiliza uamuzi wa kesi aliyowawakilisha Wabunge wanaopinga kukatwa mishahara yao na posho.
Inaelezwa kuwa Kajwang’ na Mwanasheria mwingine anayejulikana kwa jina la Miguna Miguna, ndio walikuwa wasimamizi wakuu wa tukio hilo la kumuapisha Odinga katika viwanja vya Uhuru Park.
“Maswali mengi ya Wabunge nayoulizwa yanahusu ujenzi wa Mahakama” Prof. Kabudi