Taarifa zilizoripotiwa leo Alhamisi ya October 12 2017 kuhusiana na club ya FC Barcelona ya Hispania ni kuwa inajiandaa kubadili jina la uwanja wake wa Nou Camp kwa ajili ya kuongeza kipato.
Club ya Barcelona inaripotiwa kuwa tayari imetenga dau la euro milioni 500 kwa ajili ya ukarabati wa uwanja huo ambapo ujenzi ukikamilika utakuwa na miundombinu ya kisasa na kuchukua watu 105,000 mwisho wa msimu wa 2021/2022.
Mtendaji mkuu wa club ya FC Barcelona ana imani kuwa hadi kufikia nusu ya mwaka 2018 watakuwa wamempata mdhamini watakayeingia nae mkataba wa kubadili jina la uwanja wa Nou Camp kwa ajili ya kuongeza kipato na wameanza mazungumzo na kampuni mbalimbali kubwa duniani na inatazamiwa kuwa wanaweza kuingiza euro milioni 200 kwa kubadili jina uwanja.
List ya majina 30 ya wanaowania tuzo ya Ballon d’Or 2017