Mtandao wa Twitter ni moja kati ya mitandao ya kijamii maarufu sana duniani ambao umekuwa ukitumiwa na watu wengi hasa wanamuziki, wanamichezo na wanasiasa ambapo huwa njia rahisi kuwafikia watu wao.
Kumekuwa ushindani mkubwa kwenye mtandao huo kwa watu kuongeza wafuasi ‘followers’ kutokana na kile unachokifanya ili kuwafikia ambapo mshindi wa mbio hizo ni Katy Perry ambaye ni Mwimbaji wa Pop kutoka Marekani amekuwa binadamu wa kwanza kufikisha followers 100m kwenye Twitter, kwa mujibu wa Twitter.
Katy Perry alijiunga na mtandao huo mwaka 2009 na amekuwa active tangu hapo na kutokana na kufikisha idadi hiyo mtandao wa Twitter uliamua kumpongeza kwa kuandika:>>>”Today, we #WITNESS history. Congratulations @katyperry, the first to reach 100 million followers! #LoveKaty” (Leo tunashuhudia historia. Hongera @katyperry, mtu wa kwanza kufikisha wafuasi 100 milioni #LoveKaty). – Twitter
Star mwimbaji wa Pop kutoka Marekani, Katy Perry ametajwa kuwa mtu wa kwanza duniani kupata wafuasi milioni 100 kwenye mtandao wa Twitter. pic.twitter.com/SL1DtTQU9X
— millardayo (@millardayo) June 19, 2017
Msimamo wa ACT Wazalendo baada ya Walemavu kupigwa mabomu DSM