Baada ya club ya Simba SC kumkosa kwa muda mrefu beki wake wa kati wa kimataifa wa Uganda Juuko Murshid bila kutoa sababu za msingi kama wamemuacha au la, leo September 12 2018 wametoa good news kuhusu beki huyo.
Simba SC leo wamethibitisha kuwa wapo katika maelewano mazuri na beki wao huyo baada ya kumkosa uwanjani kwa muda mrefu, kaimu Rais wa Simba SC Salim Abdallah kupitia Azam TV amethibitisha matatizo kati yao na Juuko yamemalizika.
“Tulikuwa na matatizo madogo ambayo kwa kweli tumeshayarekebisha na yeye amenithibitishia kuwa amekuja kufanya kazi, kwa sababu huyu ni mchezaji wetu na tulimsajili kwa malengo tunaamini kabisa kwamba huyu ni mtu mzima na haya ambayo ametuthibitishia anakuja kuyatekeleza kwa vitendo”>>> Salim Abdallah
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Juuko Murshid ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Uganda kilichocheza dhidi ya Tanzania game ya kuwania kufuzu AFCON 2019, Juuko awali aliripotiwa kuwa yupo mbioni kujiunga na club ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini lakini haijajulikana imeishia wapi.
Samatta amedhamiria kununua Private Jet?