Februry 27 2016 millardayo.com inakupa fursa ya kuziangalia habari 6 za siku kupitia vituo mbalimbali vya TV Tanzania.
Habari kutoka kituo cha channel 10 Wamachinga wachoma Barabara
Wafanyabiashara wadogo jijini Mbeya wamechoma moto Barabarani kupinga kuondolewa kwa vibanda vyao vya biashara
‘Wanachama wakubwa wamaduka ndio wanaotuharibia sisi maisha yetuTumemfata Meya lakini hakuwepo, tukamfata Naibu Meya tukaonana naye akatuambia tufanye kazi, tunashangaa kuamkia leo tunatoka kwenye usafi tumekuta vibanda vyetu havipo hii sio haki‘>>>Mfanyabiashara
‘Wametu ahadi tarehe 31, leo haifafika tarehe 31 wanakuja wanabomo vitu vyetu sisi walituahidi ikifaka tarehe 31 ndio watakuja kuondoa vitu vyetu hapa Kabwe‘>>>Mfanyabiashara
‘Ahmed Msangi kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kuacha kuharibu mali za umma ikiwemo kuchoma Barabara‘>>>mwandishi wa habari
Habari kutoka Clouds TV.. Wizara ya Elimu yatumbua Majipu.
Wizara ya Elimu imewasimamisha kazi watumishi watatu kwa kosa la uchapishaji mbovu wa vitabu vya kusomea kwa darasa la kwanza. ‘Watumishi Peter Mandio amabaye ni kaimu mkurugenzi wa idara ya vifaa vya Elimu, Bi. Pilli Magongo ambaye ni mwanasheria wa taasisi na Jackson Mwaigonela mkuu wa kitengo cha ununuzi na ugavi’>>> Maimuna Tarish Katibu mkuu wizara ya Elimu.
Habari kutoka Clouds TV… Uchaguzi Meya Pasua Kichwa
Uchaguzi wa kumtafuta Meya wa jiji la Dar es salaam umeshindwa kufanyika baada ya kaimu mkurugenzi wa jiji Sara Yohana kutangaza kuairishwa kwa uchaguzi huo hali ambayo imesababisha vurugu.
‘kwahiyo ninadhani umefika wakati sisi kama vyama kulirudisha swala hili kwa wakazi wa Dar es salaam, wajiandae tutawarudishia jambo lao kwasababu wao ndio walioamua madiwani wengi wawe wa UKAWA na walivyo chagua madiwani wengi walikuwa wanajua‘>>>Salim Mwalimu KaIimu katibu Mkuu wa Chadema.
Habari kutoka Clouds TV… Majambazi Sasa Kukiona
Kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya Uhalifu wa kutumia silaha kushamiri katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam Serikali imesema iko kwenye mkakati wa kulishirikisha jeshi la wananchi la Tanzania JWTZ katika kufanya msako ikiwa ni siku moja imepita tangu kutokea kwa uhalifu Mbagala.
‘Tulikuwa tumekaa hapa na wenzangu tunapiga stori ghafla tulisikia risasi zinalia tukakimbia, baada ya majambazi kuondoka tulikuta ni ujambazi umetokea‘>>>Shuhuda
‘nitazungumza na mwenzangu waziri Mwinyi tutumie ata jeshi la wananchi ili tufagie misitu yote ya mkoa wa pwani kuanzia Bagamoyo, kisarawe yote na ili tutalifanya haraka iwezekanavyo‘>>>Charles Kitwanga waziri wa mambo ya ndani ya nchi
Habari kutoka Star TV..Mafuriko Mtwara
Waziri Mkuu amewaonya wote wanaoishi mabondeni kuanza kuchukua hatua stahiki za kuondoka Mabondeni na pia Waziri Mkuu ameongelea kiwanda cha saruji Mtwara kufuatia na bei ya saruji mkoani hapo.>>>Kassim Majaliwa
‘kwahiyo ni vyema kwa wale wote mlio maeneo ya mabondeni kuanza kuondoka mabondeni kwa kuwa Mamlaka ya hali ya hewa wamesema bado kuna mvua kubwa zitazokuja mwezi wa tatu zaidi ya hizi zilizotokea‘>>>Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Pia Waziri Mkuu ameongelea bei ya saruji Mkoani Mtwara…’tutamuita atupe maelezo sahihi na kama hivyo ndivyo ataeleze kwanini, maana yakuwa na kiwanda mahali ni pamoja nakupata bidhaa hiyo kwa unafuu‘
Habari kutoka ITV... Serikali imetoa siku saba kwa kiwanda cha A to Z
Serikali imetoa siku saba kwenye kiwanda cha nguo cha A to Z cha jijini Arusha kulipa faini ya shilingi milioni 70 ambayo ilitakiwa kulipa mwezi wa tisa mwaka jana baada ya kiwanda hicho kutiririsha maji machafu.
‘narudia tena kiwanda kinatakiwa kulipa faini na ni wajibu kwa kila kiwanda kufata maagizo tunayoyatoa na kuheshimu mamlaka endapo hautafanya hivyo ndani ya siku saba tutafunga kiwanda‘>>>Luaga Mpina Naibu Waziri wa Mazingira
Ulikosa kuangalia Video ya magoli ya Yanga Vs Cercle de Joachim, Full Time 2-0 27/02/2016
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE