Ndani ya wiki hii moja ya story zilizokuwa kubwa Bongo ilikuwa ni story ya namba za simu za mastaa Fid Q na AY kuwa hacked na mtu asiyefahamika, halafu jamaa aliyehack akawa anatuma message kwa marafiki wa karibu wa mastaa hao na kuwaomba hela.
Muda mfupi uliopita, kupitia Instagram na Twitter, Fid Q na AY wameweka story ya kumkamata mtu aliyehusika kufanya uhalifu huo.
“Yule HACKER ndo huyu hapa.. Ni Mwanafunzi wa IFM.. Yuko mwaka wa pili Anaitwa AHMED….“–@fidq (Instagram)
“Huyu ndie aliyehack namba Yangu na Ya @FidQ na kuanza kutapeli watu ndio huyu,Anaitwa Ahmed anasoma IFM 2nd Year”– @AyTanzania (Twitter)
Huyu ndie aliyehack namba Yangu na Ya @FidQ na kuanza kutapeli watu ndio huyu,Anaitwa Ahmed anasoma IFM 2nd Year pic.twitter.com/d25cveJY1D
— Ambwene AY (@AyTanzania) January 17, 2015
JAMAA KASHAWAPIGA MADEMU KIBAO WA MJINI SIMU ZAO.. NA AMEKIRI KUWA YEYE NDO MWENYE ILE MICHEZO YA KUSAJILI NAMBA KWA MAJINA YA WATU MAARUFU
— #BongoHiphop (@FidQ) January 17, 2015
KUNA MADEMU KAMA SITA HIVI.. WAMEKUJA KUDAI VYAO HAPA KITUONI OYSTERBAY
— #BongoHiphop (@FidQ) January 17, 2015
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook