Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kumsomea maelezo ya awali (Ph) aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wenzake March 16, 2018.
Maelezo hayo ya awali yanatarajiwa kusomwa na Wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro mbele ya Hakimu Mfawidhi, Victoria Nongwa.
Madabida na wenzake wanakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kusambaza dawa bandia za kufubaza makali ya Ukimwi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, uzembe wa kuzuia kosa kutendeka na kusababisha hasara.
Mbali na Madabida ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu, washtakiwa wengine ni Seif Shamte ambaye ni Mkurugenzi wa Uendeshaji Simon Msoffe, Meneja Masoko na Fatma Shango Mhasibu Msaidizi.
Wengine ni Sadick Materu na Evans Mwemezi ambao ni maofisa wa Bohari Kuu ya Dawa. Watuhumiwa wote ni wafanyakazi wa Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd.
Madabida, Seif, Simon na Fatma wanadaiwa kuwa April 5, 2011 jijini Dar es Salaam waliisambazia Bohari Kuu makopo 7776 ya dawa bandia za ARV’s zenye mchanganyiko wa dawa ya stavudin 30mg +nevirapine 200mg+lamivudine 150mg.
Dawa hizo zilizotengezwa March 2011 na kuisha muda wake wa matumizi Februari 2013 huku zilionyesha kuwa ni halali wakati si kweli.
Dr. Slaa amezungumza baada ya kuapishwa na JPM Ikulu