Leo January 31, 2018 Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema Mahakama inapaswa kutoa haki bila kufungwa na masharti ya makundi yanayoweza kukwamisha haki.
Prof. Kabudi ametoa rai hiyo wakati wa kufunga maonyesho ya wiki ya sheria katika viwanja vya Mnazi Mmoja DSM.
Ameongeza kuwa mahakama zitoe fidia ipasavyo, wakuze usuluhishi baina ya watu husika katika migogoro ya wananchi kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja na kuchelewesha kesi bila sababu ya msingi na kuhakikisha mashauri yanakamilika kwa wakati.
Mbali ya kufunga wiki ya sheria, pia Prof.Kabudi alizindua Mahakama ya Kigamboni, ambapo ameeleza kuwa kuna upungufu wa mahakama na nyingine zinahitaji ukarabati.
Mwisho ameeleza kuwa Mahakama ya mwanzo na Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni imejengwa kwa siku 120 na kugharimu zaidi ya Tsh Milioni 594.
Mzee Majuto baada ya kutembelewa hospitalini na Rais Magufuli