September 23 2016 Msajili wa vyama vya siasa alitoa msimamo na ushauri wake baada ya kupokea malalamiko na kupitia maelezo ya pande zote kuhusu mgogoro wa uongozi uliopo kwenye chama cha wananchi CUF.
Baada ya upembuzi Msajili wa Vyama vya saisa Jaji Mutungi alitoa mwongozo kuwa Prof. Lipumba bado ni mwenyekiti halali wa chama hicho aidha baadhi ya viongozi na wanachama waliokuwa wamesimamishwa na wengine kufukuzwa, Jaji mutungi amesema ni wanachama halali.
Baada ya tamko hilo la Jaji Mutungi Leo September 24 2016, baadhi ya wanachama wamemsindikiza Prof. Lipumba mpaka makao makuu ya chama hicho yaliyopo buguruni jijini Dar es salaam kwa ajili ya kumkabidhi ofisi kama mwenyekiti wa halali wa chama hicho.
Baada ya wanachama kufika eneo zilipo ofisi hizo geti lilikuwa limefungwa na walinzi hivyo iliwabidi kuruka ili kulifungua kwa ndani na baada ya kuingia ofisini Prof Lipumba ameyazungumza haya
>>>’mimi sina matatizo ya kuzungumza na wanachama wote wa CUF laikini nitafanya kazi kama mwenyekiti lakini kuna mambo inabidi yarekebishwe ndani ya chama nitakapokaa vizuri nitayafanyia marekebisho yanayohitajika lakini tutafuata katiba na kanuni za chama kuhakikisha kwamba tunakijenga chama imara’
Baadhi ya wanachama CUF wafika makao makuu DSM kumkabidhi ofisi Lipumba baada ya tamko la msajili wa vyama kumtambua kama mwenyekiti halali pic.twitter.com/CjLNCqDkpd
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
#MillardAyoUPDATES Baadhi ya wanachama CUF walivyoruka geti ili kumfungulia Prof. Lipumba baada ya geti hilo kufungwa kwa ndani na walinzi pic.twitter.com/aq3k3GoDiU
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
#MillardAyoUPDATES Prof. Lipumba baada ya kuingia ofisini amesema atafanya kazi na uongozi ambao walichaguliwa na wanachama ktk mkutano mkuu pic.twitter.com/LTxWMLJw91
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
ULIKOSA MAJIBU YALIWAHI KUTOLEWA NA MTATIRO KAMA WATAWEZA KUKAA MEZA NA PROF. LIPUMBA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI