Mahakama ya Wilaya ya Tanga katika kesi Na.78/2020 mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Tanga Majani tarehe 04 Januari, 2021 imemuhukumu mtuhumiwa Haji Akida kifungo cha miaka thelathini (30) jela kwa kosa la kusafirisha dawa za Kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 0.13
Kesi hii imeendeshwa na Mwendesha Mashtaka Elizabeth Muhangwa.
Wakati huo huo Mahakama ya Wilaya ya Tanga imewatia hatiani watuhumiwa Julius John Mkiji na Julius Stephano Mtoi na kuwahukumu kifungo cha miaka thelathini (30) jela kila mmoja kwa makosa ya Ulawiti.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali Elizabeth Muhangwa aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa washtakiwa ili iwe fundisho kwa wote wanaotarajia kutenda Uhalifu kama huo.