February 25 mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Manara ameingia kwenye headlines baada ya kuamua kuweka wazi lililo moyoni mwake na kumtuhumu afisa habari wa klabu ya Dar Es Salaam Young African Jerry Muro kuwa anawatolea maneno ya kashfa na matusi viongozi wa Yanga.
Manara ameingia kwenye headlines baada ya kukaa kimya muda mrefu, kwa kile alichouwa anakiamini kuwa shirikisho la soka Tanzania TFF watamchukulia hatua za kidhamu kama walivyoahidi “Kubwa lililonifanya niwaite waandishi, ni kuhusu malalamiko ya Simba kwa matusi, kejeli, dharau na majigambo yasio na lazima ya msemaji wa Yanga (Jerry Muro), lakini TFF hawajachukua hatua yoyote, ila sasa Simba tunasema tutachukua hatua kama TF wasipo mchukulia hatua”
Huyu hapa Haji Manara akieleza kila kitu
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE