Leo September 24, 2020 Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amesema, fedha zote za miradi zipo kwenye bajeti, zinapitishwa Bungeni kila mwaka na hakuna usiri wowote.
Amesema, fedha za miradi yote inayotekelezwa nchini zipo na zimetengwa kwa mujibu wa Sheria na kwamba miradi hiyo imelenga kuboresha maisha ya Watanzania.
Amezungumzia madai ya ndege kununuliwa kwa siri bila bajeti na kusema ununuzi ulifanywa kwa mujibu wa Kifungu kipya cha 65A cha Sheria ya Ununuzi wa Umma (marekebisho ya 2016).
“Kama kuna mtu alikuwa na Wakala wake mfukoni katika ununuzi wa hizi ndege imekula kwake, Serikali imenunua moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji wanaojulikana kimataifa kama Boeing na Bombardier na Sheria inaruhusu hivyo na ilipata bei ya chini kuliko hata zile zilizoainishwa kwenye tovuti zao” Abbas