Waziri Mkuu wa Israel, Binjamin Netanyahu Jumapili alikataa shinikizo la kimataifa la kusitisha vita huko Gaza katika hotuba kali ya kuadhimisha kumbukumbu ya kila mwaka ya mauaji ya Holocaust nchini humo, akisema: “Ikiwa Israeli italazimishwa kusimama peke yake, Israeli itasimama peke yake.”
Ujumbe huo, uliotolewa katika mazingira ambayo kwa kawaida huepuka siasa, ulilenga kwaya inayokua ya viongozi wa dunia ambao wamekosoa adha kubwa iliyosababishwa na mashambulizi ya kijeshi ya Israel dhidi ya wanamgambo wa Hamas na wamezitaka pande hizo kukubaliana kusitisha mapigano.
Netanyahu amesema yuko tayari kwa makubaliano ambayo yatasitisha karibu miezi saba ya mapigano na kuwarudisha nyumbani mateka wanaoshikiliwa na Hamas.
Lakini pia anasema bado amejitolea kufanya uvamizi wa mji wa kusini wa Gaza wa Rafah, licha ya upinzani mkubwa wa kimataifa kwa sababu ya zaidi ya raia milioni 1 waliokusanyika huko.
“Ninawaambia viongozi wa dunia: Hakuna shinikizo la kiasi gani, hakuna uamuzi wa jukwaa lolote la kimataifa litakalozuia Israeli kujilinda,” alisema, akizungumza kwa Kiingereza. “Siyo tena sasa.”
Yom Hashoah, siku ambayo Israeli inaadhimisha kama ukumbusho wa Wayahudi milioni 6 waliouawa na Ujerumani ya Nazi na washirika wake katika mauaji ya Holocaust, ni moja ya tarehe muhimu zaidi kwenye kalenda ya nchi. Hotuba katika sherehe hizo kwa ujumla huepuka siasa, ingawa Netanyahu katika miaka ya hivi karibuni ametumia fursa hiyo kumkashifu adui mkuu wa Israel Iran.