Umoja wa Mataifa umethibitisha kufungwa kwa maduka yote ya mikate na unga kaskazini mwa Gaza, huku kukiwa na uhaba wa maji na mafuta.
Uhaba wa unga ulitokea baada ya mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa kushindwa kupeleka chakula chochote huko huku kukiwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya mabomu na uvamizi wa vikosi vya Israel.
Kusini mwa Gaza, Umoja wa Mataifa ulisema kuwa ni viwanda tisa pekee vya kuoka mikate ambavyo bado vinafunguliwa “mara kwa mara”, kutoa mkate kwenye makazi wakati unga na mafuta zinapatikana.
Tangu Oktoba 21, jumla ya lori 569 zimeingia Gaza kupitia kivuko cha Rafah Kusini mwa Gaza, lakini maafisa wa Palestina wanasema hakuna hata moja iliyofika Kaskazini.
Kabla ya vita, idadi ya lori zinazoingia kila siku ilikuwa kati ya 750 na 850
Tel Aviv ilianzisha vita baada ya makundi ya upinzani ya Gaza kuendesha Operesheni Al-Aqsa Storm, operesheni yao kubwa zaidi dhidi ya taasisi inayoikalia kwa miaka mingi.
Taarifa hiyo kutoka kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kutoa misaada katika maeneo ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu inakuja baada ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Gaza kusema kuwa Maduka yote mikate katika Jiji la Gaza na Kaskazini mwa Gaza yalikuwa yamefungwa Jumatatu.