Leo February 9,2020 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres amesema kuna uhusiano kati ya mabadiliko ya hali ya hewa na uvamizi wa nzige nchini Ethiopia.
Guterres amesema uvamizi huo ni mbaya zaidi kutokea katika Ukanda wa Afrika Mashariki kwa takriban miaka 25, na kuna wasiwasi kuwa janga hilo linaweza kusababisha baa la njaa.
–
Mbali na Ethiopia, Nchi nyingine zilizotajwa kuathirika na uvamizi wa nzige ni Kenya, Eritrea, Sudan na Somalia.
Aidha, imetahadharishwa kuwa, kuna uwezekano wadudu hao wakasambaa hadi Uganda na Sudan Kusini.