Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtaka mbunge wa Kawe, Halima Mdee na mbunge wa Bunda, Ester Bulaya kujieleza Januari 21, 2020 kwanini dhamana zao zisifutwe kutokana na kukiuka masharti ya dhamana.
Pia mahakama hiyo imepanga kuwahoji wadhamini wa wabunge hao kuhusu kufutwa kwa dhamana zao.
Hatua hiyo inatokana na hoja iliyoibuliwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba akidai kwamba mbunge Mdee na Bulaya wameonekana wakiwa nje ya mipaka ya Tanzania bila kuwa na kibali.
Kutokana na hoja hiyo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 21, 2020 ili wabunge na wadhamini wao wajieleze kuhusu dhamana.
MAOMBI YA UMILIKI WA SILAHA YAMSHTUA RC KILIMANJARO, WAMO VIONGOZI WA DINI