Hamas imedai kuwa mateka saba waliuawa katika shambulizi la anga la Israel kwenye kambi ya wakimbizi kaskazini mwa Gaza hapo jana.
Kundi hilo la wapiganaji lilisema kuwa mateka watatu walikuwa wageni.
“Vikosi vya Al-Qassam vinatangaza kuuawa kwa wafungwa wake saba wa raia katika mauaji ya Jabalia jana, wakiwemo watatu waliokuwa na hati za kusafiria za kigeni,” iliandika kwenye Telegram.