Ismail Haniyeh, mkuu wa kundi la muqawama la Palestina Hamas ameuawa nchini Iran, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Hamas na maafisa wa Iran.
Hamas ilisema kiongozi wake aliuawa mapema Jumatano kufuatia uvamizi wa Israel uliolenga makazi yake mjini Tehran.
Katika taarifa, kundi hilo limeomboleza kifo cha Haniyeh, 62, ambaye limesema aliuawa katika “uvamizi wa kihaini wa Wazayuni kwenye makazi yake mjini Tehran baada ya kushiriki katika sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa Iran.”
Haniyeh, mtu mashuhuri katika kundi la kisiasa na upinzani la Palestina, amekuwa mtu muhimu kabla na wakati wa vita vya mauaji ya halaiki ya Israel dhidi ya Gaza iliyozingirwa.
Serikali ya Iran ilitangaza uchunguzi kuhusu mauaji hayo, huku matokeo yakitarajiwa kutolewa hivi karibuni.